Skip to main content

30 mei 2015


Vidokezo
--Mwanasiasa aapa kuendelea kuwasaidia watoto mayatima eneo bunge la kitutu masaba kaunti ya Nyamira  Nyamira
--wazazi waombwa  kuchukua vyeti vya kuzaliwa  kutoka kwa ofisi ya kuwasajili  kwa kuwa viko tayari  kwa wanao.
---Msitumiwe na wanasiasa vijana kutoka eneo bunge la Kitutu masaba kaunti ya nyamira waambiwa na mbunge wao.
  ……………..
1] Mwanasiasa  Ogeto Swanya  kutoka eneo bunge la Kitutu Masaba ameapakuendelea kuwasaidia mayatima wa eneo bunge hilo kupata elimu.
Akiongea Ijumaa katika  hafla  ya mazishi ya mama  Mary Simeon kijiji cha Riamisiani wadi ya Gesima Ogeto alisema anataka kuinua kiwango cha masomo katika eneo bunge hilo.
Aidha, aliwaomba wakazi wote kushirikiana  ili kuinua viwango vya masomo  kwa kuwa ndio itasaidia kupata viongozi wa kesho.
Ogeto alisema kuwa atatembelea shule zote katika eneo hilo huku akiwatabua watoto mayatima.
Kwa upande mwingine aliwaomba viongozi waliomamlakani kwa sasa kuwasaidia wananchi ili kuinua viwango vya maendeleoo katika eneo bunge la Kitutu Masaba.
Alimwomba mwakilishi wa wadi ya Gesima Kennedy Nyameino  kukarabati baadhi ya barabara ambazo zimeharibika katika wadi ya Gesima ili kuwasaidia wakulima na wafanyibiashara.
 Ogeto pia alidokeza kuwa ameongea na Nyameino kuhusu ukarabati wa barabara ya Matunwa –Kiamitengi  na ile ya  Gesima – Esani- Magombo.
2] Mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba kaunti ya Nyamira, Timothy Bosire amewaomba vijana wa eneo bunge hilo kutotumiwa na wanasiasa kurudisha maendeleo ya eneo hilo nyuma.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika eneo la Rigoma, mbunge huyo alisema kuna wanasiasa wanawatumia vijana wa eneo hilo ili kukosoa uongonzi wake.
Wanasiasa hao wanadai kuwa hafanyi maendeleo katika eneo hilo jambo ambalo amekerwa nalo na kuomba vijana kushirikiana naye kuinua maendeleo ya eneo hilo.
Hii ni baada ya baadhi ya vijana wa eneo hilo kujitokeza na kuchukua hatua ya kulima barabara za eneo hilo huku wakisema zikarabatiwe haraka.
Bosire aliwahakikishia wakaazi wa eneo hilo kuwa hakuna pesa za kuzikarabati barabara hizo katika hazina na kusema pindi pesa hizo zitaingia kwa hazina ya ustawi maeneo bunge, barabara hizo zitakarabatiwa kikamilifu.
Wakati huo huo, mbunge huyo aliwaomba vijana  kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ili kuhakikisha maendeleo yamefanywa na kutimizwa  kikamilivu na kujiimarisha na  kujiendeleza kimaisha badala ya kutumiwa na wanasiasa ambao hawana maono ya siku za usoni
3] Katibu mkuu  wa ofisi ya kusajili vyeti vya kuzaliwa katika wilaya ya Kisii ya kati kaunti ya Kisii, Mattews Ayota amewaomba wazazi kuchukua vyeti vyao kutoka ofisi hiyo.
Hii ni baada ya vyeti zaidi ya 3,000 kubaki katika ofisi hiyo kwa muda mrefu bila kuchukuliwa.
Akizungumza na na kuitu hiki  katibu huyo alisema vyeti hivyo vimekuwa kwa ofisini mwake kwa muda mrefu bila kuchukuliwa jambo ambalo limemshangaza sana.
Katibu huyo amewaomba wazazi wote walioenda kwa ofisi hizo na kujaza fomu za vyeti hivyo kuenda kuvichukua na kuviweka mahala pazuri kwani vimekuwa kwa ofisi hiyo kwa muda mrefu sasa.
 
Katibu huyo pia alisema walimu wa shule ndio huwatuma wanafunzi kuwambia wazazi wao waende  kujaza fomu hizo.
Alisema kuwa wazazi hao hupanga foleni ndefu na hata kurejea siku ya pili lakini wanapomaliza shughuli ya kujaza fomu hizo hawashughuliki kuchukua vyeti hivyo.
4] Wakulima wa majani chai kutoka Tendere, wilaya ya Ogembo kaunti ya Kisii wameombwa wasing'oe zao hilo na kupanda michai ya gredi 1 ili kuimarisha bei ya zao hilo ambayo inafifia.
Hii ni mojawapo ya harakati za kufufua matumaini ya wakulima wengi wa zao hilo, ambao wamekuwa wakiling'oa huku wakilalamikia malipo duni kutokana na zao la majani chai.
Kwenye mahojiano na mwenyekiti wa vituo vya kupima majani chai vya kiwanda cha kusaga majani chai cha Tendere kilichoko Ogembo, John Nyabuto aliwaomba wakulima wa eneo hilo kuacha kung’oa zao hilo na kuanza kushiriki makongamano yanayoandaliwa na kamati kutoka idara ya kilimo na kufaidi utaalamu jinsi ya kupanda mazao ya ubora wa juu.
Kilimo cha majani chai kimekuwa kikififia kwa siku za hivi karibuni kwenye maeneo mengi ya Kisii na Nyamira, ambapo wengi wa wakulima wa maeneo hayo wamehiari kuanza kung’oa mimea yao, na kuingilia kilimo tofauti na kushtumu usimamizi wa mamlaka majani chai nchini kuwadhulumu.
 
5] Naibu kamishna wa Kaunti ya Kisii Phillip Soi amewahakikishia wakaazi wa wadi ya Magenche Kaunti ya Kisii kuwa usalama utawekwa dhidi yao kikamilifu.
Haya yanajiri baada ya wakaazi hao kuenda hadi ofisi yake iliyoko mjini Kisii siku ya Alhamisi kulalama kuwa wamehofiya usalama wao baada ya baadhi ya viongonzi wa eneo hilo ambao ni machifu na manaibu wao kutengeneza kikundi cha vijana kuwatisha wakaazi hao dhidi ya uongonzi wa eneo hilo..
Wakati huo huo, naibu kamishna wa Kisii Phillip Soi alisema hatua za haraka zitachukuliwa dhidi yao ili kuhakikishiwa usalama wao na kuzuia ugomvi huo katika mipaka yao hasa katika mpaka wa Wakisii na Wamaasai.
Katika mpaka huo kumeshuhudiwa wizi wa mifugo kwa muda mrefu sasa lakini suluhu itapatikana hivi karibuni hayo ni kwa mujibu wa naibu kamishna.
                                                                        Asante sana 
                                                                           By Brighton Makori

Comments

Popular posts from this blog

What you need to Know about EDV 2023 (US Green card lottery program)

Success Africa ON AGR with Sylvester Oluoch hosted by Arphaxad Nyabuto

WHAT WAS DP RUTO'S MESSAGE TO KENYANS, EBIBANDA GOSAMBWA NA GOTAGORWA I...