Skip to main content
Mwanasiasa amtaka mbunge wa Kitutu Chache kaskazini kuheshimu wanasiasa wengine
 Mbunge wa Kitutu Chache kaskazini Jimmy Nuru Angwenyi. Ameombwa kuwaheshimu wanasiasa wengine katika Kaunti ya Kisii.

Mwanasiasa aliyewania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini kaunti ya kisii, James Atandi amemtaka mbunge aliye mamlakani katika eneo bunge hilo Jimmy Nuru Angwenyi kuheshimu wanasiasa wengine walio katika mamlaka na wale wasio mamlakani.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika hafla ya mazishi ya ajuza Jeruza Orure yalioyofanyika katika kijiji cha Kemanko, Atandi alimtaka mbunge wa eneo hilo kutoharibia majina wanasiasa wengine na kufanya kazi aliyochaguliwa kufanya.

"Sisi wanasiasa ni maadui kwa wanasiasa wengine. Ni jukumu la kila mwanasiasa kuheshimu mwanasiasa mwingine. Naomba mbunge wa eneo hili kuniheshimu ingawa zikuchaguliwa. Wakati wangu utafika na mwaka 2017 nitasimama tena. Angwenyi asije akaniharibia jina kwa mikutano mingine,”alisema Atandi.

Aidha, mwanasiasa huyo aliomba mbunge wa eneo hilo jimmy Angweny kuonyesha uwazi wakati pesa za msaada wa karo kutoka hazina ya CDF zinapopokezwa kwa wanafunzi wa eneo bunge hilo.
“Kila mwanafunzi anastahili kupokezwa pesa za msaada wa karo lakini kuna maneno ambayo hufanyiwa mvunguni. Wale waliojulikana wakati wa kampeini watoto wao ndio hufaidika na hupokezwa pesa hizo. Niko na fomu nyingi ambazo zinaonesha mambo hayo na zinafichua ukweli wa pesa hizo. Nitayafichua mambo hayo hivi karibuni ili yajulikane,” aliongeza Atandi.
Kwa upande mwingine watu waliokuwa katika mazishi hayo walimshangilia mwanasiasa huyo huku wakisema ni ukweli yale aliyokuwa akisema haswa kuhusu ugawaji wa pesa za msaada wa karo katika eneo bunge hilo.

Kanisa la Kiadventista kuwafadhili akina mama Makanisa ya SDA kwa ushirikiano na shirika la kifedha la World Vision Fund yanalenga kuwapa kina mama uwezo wa kujisimamia kiuchumi na kulea jamii kwa maadili yafaayo.

Wakulima wa miwa kutoka Kisii wahimizwa kujiandikisha kwenye vyama
Waziri wa Kilimo Kaunti ya Kisii Vincent Sagwe. Amewahimiza wakulima wa miwa katika eneo bunge la Mogirango Kusini, kujiandikisha kwenye makundi ya jumuia.
Katika hatua mojawapo ya kuwapa nguvu wakulima wa miwa katika eneo bunge la Mogirango Kusini, wizara ya kilimo imeanza uhamasisho miongoni mwa wakulima kutoka eneo hilo kujiandikisha kwenye makundi ya jumuia.

Hatua hiyo itafanya iwe rahisi kwao kuweka mwafaka kati yao na kampuni za kusaga miwa.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika afisi yake, waziri wa Kilimo Bwana Vincent Sagwe, alisema kuwa wakulima wakiwa katika vyama itakua rahisi kupata mikopo.

Aliwataka wakulima kupanda miwa kwa wingi ili ziwafae kimapato na kuendeleza uchumi wa eneo hilo ambalo limesahaulika kwa muda mrefu.

Sagwe alisema hii ni nafasi yao ya pekee ya kupata kazi katika viwanda kama hivyo.
Dhamira hii inalenga zaidi kiwanda cha miwa ambacho kitajenywa katika eneo bunge hilo sehemu ya msitu wa Nyangweta hivi karibuni.


MWANDISHI WA VITABU VYA HADITHI AWASHUTA WANASIASA KUIMARISHA MASOMO KISII

Mwandishi wa vitabu vya hadithi bwana Joseph Nyatwong`I awataka wanasiasa kutoka maeneo ya kisii kuwajibika na kuimarisha viwango vya masomo kaunti ya kisii na nyamira.

Akiongea hiyo jana katika shule ya upili ya Naikuru aidha alisema baadhi ya wanasiasa hao wanajaribu lakini bado hawachafikia viwango vile ambavyo vinahitajika kuimarisha sekita ya elimu nchini wakianza na maeneo yao ya uwakilishi bunge. Pia alisema ni jukumu la wanasiasa kubadilisha namna au jinzi wakaazi wa kisii wamekua wakifanya au kuendelesha sekita hiyo ya masomo.

``… ni wakati tunafaa kuwajibika na kufanya yale yote tunayohitajika kufanya hili kuinua viwango vya masomo kisii na Kenya nzima kwa jumula, elimu ndio shamba na urithi wowote ule mzazi anaeza mpa mwanaye usioisha na uwa wa milele na ukitumika vizuri urithi huu basi matunda yake hayaisha milele kwa hata vizazi vijavyo kamwe….’’ Nyatwong`I alidai

Amewataka pia wasomi walio maeneo ya kisii kutembelea shule zote za maeneo hayo mara kwa mara na kuwa na masungumzo na wanafunzi hili kuwapa motisha na mwelekeo mwafaka kimasomo kwa matokeo ya viwango vya juu na kupendaza kutoka maeneo hayo ya kisii.

Comments

Popular posts from this blog

Success Africa ON AGR with Sylvester Oluoch hosted by Arphaxad Nyabuto

What you need to Know about EDV 2023 (US Green card lottery program)

Etaya Yokire Bomachoge (Job Nyangenya Bwomanga) by Mr Ong'eng'o