Prepared by Denis zadock news anchor yard fm 28 th may 2015 -- Imetimu saa 4.oopm wakati wa kupokea habari za yard fm lakini kwanza tupate mkhutasari wake -- Ukidhani umeathirika na ugonjwa wa saratani usikonde kuna kupimwa na kushugulikiwa kikamilifu asema waziri wa afya kisii saraha omache -- Tuliamurishwa kufunga shule kutokana na hali mbaya ya vyoo asema mwalimu mkuu wa shule ya gesere D.O.k -- Mwakilishi wa wadi Fred menge amrudishia asante rais Kenyatta kwa kupunguza gharama ya stima -- Hatutakubali wakulima kuendelea kutezeka afisa wa benki ya dunia Charles mochama aambia serikali ya Nyamira -- Hujambo na karibu naitwa ………………….. 1 Maafisa wa afya kutoka kaunti ya Kisii wamefunga Shule ya msingi ya Gesere D.O.K iliyoko wadi ya Ibeno kaunti ya Kisii hadi wakati usiojulikana kufuatia na vyoo vya shule hiyo kuwa katika hali mbaya. Akizungumza na waandishi wa habari jana mwalimu mkuu wa shule hiyo Velste...