--Ni wakati wa kupokea habari za yard fm NA AGR FM lakini kwanza mkhutasari wake. ---Ni haki yetu kutengenezewa barabara wakaazi wa Nyaribari Masaba wasimama kidete ----Lazima gavana atueleze yale ametekeleza kimaendeleo kwa kaunti ya Nyamira mbunge wa Kitutu Masaba Timoty Bosire akariri ----Soko la Gesusu kupata sura mpya karibuni ---Wanahabari wa Kisii wajipata matatani tena kwa kutoa habari si halisi 1 wakaazi wa eneo Bunge la Nyaribari Masaba, Kaunti ya Kisii waliandamana hiyo jana, kulalamikia hali mbaya ya barabara ya kutoka makutano ya Geteri kuelekea soko la Geteri ambayo kwa sasa haipitiki. Waendeshaji Bodaboda waliojawa na gadhabu walilalamikia hali duni ya barabara hiyo ambayo kwa sasa haipitiki kamwe kufuatia mvua nyingi inaendelea kunyesha katika sehemu za Kisii. Vijana hao wakiongozwa na mwenyekiti wa Bodaboda wa eneo hilo Mong’eri Nyabicha walichukua hatua ya kupanda mgomba wa ndizi katika baraba...