Mwanasiasa amtaka mbunge wa Kitutu Chache kaskazini kuheshimu wanasiasa wengine Mbunge wa Kitutu Chache kaskazini Jimmy Nuru Angwenyi. Ameombwa kuwaheshimu wanasiasa wengine katika Kaunti ya Kisii. Mwanasiasa aliyewania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini kaunti ya kisii, James Atandi amemtaka mbunge aliye mamlakani katika eneo bunge hilo Jimmy Nuru Angwenyi kuheshimu wanasiasa wengine walio katika mamlaka na wale wasio mamlakani. Akizungumza siku ya Alhamisi katika hafla ya mazishi ya ajuza Jeruza Orure yalioyofanyika katika kijiji cha Kemanko, Atandi alimtaka mbunge wa eneo hilo kutoharibia majina wanasiasa wengine na kufanya kazi aliyochaguliwa kufanya. "Sisi wanasiasa ni maadui kwa wanasiasa wengine. Ni jukumu la kila mwanasiasa kuheshimu mwanasiasa mwingine. Naomba mbunge wa eneo hili kuniheshimu ingawa zikuchaguliwa. Wakati wangu utafika na mwaka 2017 nitasimama tena. Angwenyi asije akaniharibia jina kwa mikutano mingine,”alisema Atandi. Ai...