-- Ni wakati wa kupokea habari za YARD fm na AGR lakini kwanza tupate mkhutasari wake
Maandamano si suluhu gavana Ongwae ambia wakaazi wa kisii
--Tunahitaji pesa nyingi katika mashindano ya tamasha za mziki asema naibu mwenyekiti evans Gesanda
--Serikali ya Nyamira yaombwa kuongeza pesa zaidi kwa sekta ya afya
Mzipozingatia usafi mtaathiriwa na funza mhudumu wa afya katika jamii Kepha kengoina awaonya wakaazi wa mwembe
--Kizungumkuti chazuka kati ya afisa wa polisi na madereva wa teksi mjini Kisii
Habari kamili
1 Gavana aomba wakazi kutafuta sululu wakatijambo mbaya linapotokea bali si kuandamana-Kisii
Wakazi wa kaunti ya Kisii wameombwa kutoandamana wakati kuna jambo mbaya linapotokea katika maeneo mbalimbali ya Kuanti hiyo kwani hiyo si suluhu .
Akiongea na wananchi wa eneo bunge la Bochari kaunti ya Kisii walioandamana hii leo hadi ofisi za Gavana wa kaunti ya Kisii zinazopatikana mjini Kisii Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae, aliwaomba wakazi hao wasikuwe na tabia ya kuaandamanaa kwani maandamano si suluhu ya kuleta maendeleo katika kaunti ya Kisii,
Wakazi hao walioandamana hadi ofisi ya Gavana kulalamikia kuwa serikali ya kaunti ya Kisii imenunua shamba la kutupa taka chafu [dumping site] katika eneo hilo jambo waliosema kuwa hawataki uchafu katika sehemu hiyo ambayo hutoa harufu mbaya ,madai ambayo serikali ya kaunti hiyo ilikana na kusema kuwa wao hawajanunua shamba katika eneo hilo.
Kulingana na Gavana James Ongwae aliwakikishia wakazi hao kuwa serikali ya kaunti ya Kisii hajijanunua shamba lolote katika eneo hilo.
Aidha ,aliongezea kuwa walitangaza kuwa mwenye aliyekuwa na shamba la kuuza ndipo walipata mtu mmoja kutoka eneo hilo aliyetangaza kuwa alikuwa na shamba na serikali ya kaunti ya Kisii lazima ingewahusisha wakazi kubaini kama watakubali shamba hilo kununuliwa na kutumiwa kuwekwa uchafu.
2 Naibu mwenyekiti wa mashindano ya tamasha za muziki katika shule zote za msingi katika kaunti ya Kisii, Evans Gesanda ameomba serikali kuu kuongeza pesa kwa mashindano hayo ya tamasha ili kufikia kile kiwango kinahitajika katika tamasha hizo ambazo hufanyika kila mwaka.
Akizungumza na wanahabari katika shule ya msingi ya Kisii, kulipokuwa na tamasha hizo kwa siku tatu mfululizo, naibu mwenyekiti huyo alisema pesa ambazo hupokea kutoka kwa serikali kuu ni kidogo na hazitoshi kamwe kwa tamasha hizo.
Aidha, naibu huyo alisema pesa zikiwa za kutosha hata wale ambao wanasimamia tamasha hizo na wale wanafunzi wanahusika katika tamasha hizo watakuwa na motisha katika mashindano hayo na michezo hiyo itafanyika vyema zaidi.
3 Mwenyekiti wa chama cha kupambana na ugonjwa wa ukimwi[NationalAids Control council] katika kaunti ya Nyamira John Kimani ameomba serikali ya kaunti hiyo kuongeza pesa zaidi katika sekta ya afya baada ya kusemekana kuwa madaktari wa kuwahudumia wagonjwa ambao wameathirika na ukimwi hupitia changamoto chungu nzima kwa ukosefu wa pesa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Nyamira mwenyekiti huyo alisema madaktari hupata shida nyingi wanapowahudumia wagonjwa wa ukimwi kwa kukosa pesa za kutosha katika sekta ya afya ambazo zitashughulikia mahitaji yote ya kuwahudumia wagonjwa.
Wakati uo huo mwenyekiti huyo alisema kuna haja ya kuwatafuta wafadhili wengine ambao wataweza kushirikiana na sekta ya afya ili sekta hiyo kufanya vyema haswa kwa kuwahudumia watu wale wameathirika na ugonjwa wa ukimwi kwa kufadhili sekta hiyo.
Serikali ya kaunti ya Nyamira kupitia bunge la kaunti hiyo imeombwa kuingilia kati suala hilo ili kupata suluhu halisi ili pesa ziongezewe kwa sekta ya afya.
Serikali ya kaunti ya Nyamira kupitia bunge la kaunti hiyo imeombwa kuingilia kati suala hilo ili kupata suluhu halisi ili pesa ziongezewe kwa sekta ya afya.
4 Wakazi wa mtaa wa Mwembe, Kaunti ya Kisii wameombwa kuzingatia usafi kila kuchao ili kujingika kutokana na kuvamiwa na funza.
Akiongea na wakazi katika mtaa wa Mwembe eneo bunge la Kitutu Masaba, mhudumu wa afya ya Jamii katika kaunti ya Kisii Kepha King’oina alichukua fursa hiyo na kuwaomba wakazi hao kuzingatia usafi ili kujingika kutoka na funza hao.
Aidha, alisema kuwa wao kama wahudumu wa afya wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa funza, ambazo zimekuwa matatizo kwa jamii hazipo tena.
Akiongea na wakazi katika mtaa wa Mwembe eneo bunge la Kitutu Masaba, mhudumu wa afya ya Jamii katika kaunti ya Kisii Kepha King’oina alichukua fursa hiyo na kuwaomba wakazi hao kuzingatia usafi ili kujingika kutoka na funza hao.
Aidha, alisema kuwa wao kama wahudumu wa afya wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa funza, ambazo zimekuwa matatizo kwa jamii hazipo tena.
5 Afisa mmoja wa Polisi katika kitengo cha trafiki alizua kioja hiyo jana alipotaka kuingia kwa lazima katika gari moja ya taksi mjini Kisii.
Kisa hicho kiliwasababisha madereva wa kituo hicho kilichoko karibu na duka la Jumla ya Shivling mkabala na mkahawa wa kifahari wa New Zonic kutaka kuchukua hatua ya kumchapa Polisi huyo kwa kudai kuwa kitendo chake ni kinyume na sheria.
Kwa mujibu wa mmoja wa madereva hao Charles Mokaya, alidai kuwa Polisi huyo wa trafiki alianza kuingia katika mojawapo ya magari yao huku akitaka kumtoa dereva aliyekuwa ndani kwa fujo, hali ambayo iliwakera baadhi yao na kutaka kumchapa. Madereva hao ambao walikuwa wameanza kujikusanya pamoja na watazamaji wengine waliokuwa wakipita walighadhabishwa na kitendo hicho huku wakiwaomba Maafisa kuwa na utaratibu wa kusuluhisha jambo linapozuka miongoni mwa madereva na wahudumu wengine wa barabara.
Kisa hicho kiliacha wengi na masuali ikizingatiwa kuwa ni majuzi tu afisa mmoja wa trafiki alidaiwa kumpokonya dereva funguo za gari na baadaye kusababisha ajali kwa kuwaua wanafunzi na mfanyakazi wa taasisi ya Sayansi ya Teknolojia ya Gusii (GIT) ambapo ilizua ghasia zilizodumu kwa siku nne.
Imeandaliwa na Denis zadock
KIMATAIFA
Bunge Libya lawataka wananchi kupambana na ugaidi
Spika wa Bunge halali la Libya amewataka wananchi kuungana kwa ajili ya kupambana na ugaidi. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema, kuwa macho katika kulinda na kudumisha umoja wa kisiasa na kitaifa wa Iraq kuna umuhimu mkubwa mno
Gazeti la Lebanon limefichua barua ya siri iliyotumwa na utawala wa Aal- Saud nchini Saudia kwa serikali ya Ufaransa, ukiitaka serikali hiyo isimamishe mpango wake wa kulipatia silaha jeshi la Lebanon. Gazeti la as-Safir limekinukuu chanzo kimoja cha serikali ya Ufaransa kwamba, Riyadh iliitumia barua hiyo ya siri serikali ya Paris katikati ya mwezi uliopita ikiitaka kusitisha mpango wa ukabidhianaji silaha wenye kugharimu kiasi cha dola bilioni tatu kwa jeshi la Lebanon. Ni vyema ifahamike kuwa, makubaliano baina ya Ufaransa na Lebanon kwa ajili ya kulipatia silaha jeshi la nchi hiyo ya Kiarabu, yalitiwa saini mwezi Februari mwaka huu huko huko nchini Saudia
Wanachama kadhaa wa al-Shabab wauawa Somalia
Burundi yaridhia kutumwa waangalizi wa uchaguzi
UN yakosoa matamshi ya Rais wa Sudan Kusini
Mkuu wa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa amekosoa matamshi ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye amesema wanajeshi wa kofia ya buluu katika nchi yake ni majasusi. Hervé Ladsous amesema walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Sudan wanafanya juhudi kubwa za kulinda raia na kwamba matamshi ya kiongozi wa nchi hiyo yamepokewa kwa masikitiko makubwa na umoja huo. Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema machafuko ya Sudan yameongeza mashinikizo kwa walinda amani kwani zaidi ya wakimbizi 136 000 wanapewa hifadhi kwenye vituo mbalimbali vya UN katika nchi hiyo na kwa mantiki hiyo, serikali ya Juba inafaa kuwapongeza wanajeshi wa kofia ya buluu badala ya kuwadhalilisha.
Jana Jumatano Rais wa Sudan Kusini alisema walinda amani kadhaa wa UN wamekamatwa wakipiga picha maeneo kadhaa ya nchi na kutaja kitendo hicho kuwa ni ujasusi.
China yawazuia Waislamu wa Xinjiang kufunga Saum
Serikali ya China imepiga marufuku wanafunzi, walimu na watumishi wa umma katika eneo la Xinjiang lenye Waislamu wengi kutekeleza ibada ya Saumu kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
Comments
Post a Comment