--Waziri wa fedha Henry Rotich asoma Bujeti ya mwaka wa 2015-2016 . --tunaomba serikali kuwatia mbaroni wakimbizi ghushi asema mwenyekiti Nemuel Momanyi --ni haki yetu hatutarudisha sare za kazi wafanyikazi wa nyamira wasimama kidete. --kamishena wa kisii chege mwangi kuzuru eneo la gesure hivi karibuni 1 Bajeti ya mwaka wa 2015-2016 imesomwa hii leo katika ukumbi wa bunge la kitaifa ikiwasilishwa na waziri wa fedha nchini Henry Rotich. Bajeti hiyo ya pesa taslimu shillingi trillion mbili itanufaisha baadhi ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kutengeneza barabara kutengewa kiwango kikubwa cha pesa. Hii ni mara ya pili bajeti kusomwa chini ya uongonzi wa serikali ya Jubilee huku wakenya wengi walikuwa wanatarajia bei ya bidhaa kushuka na hata masuala muhimu ikiwa suala la kuimarisha usalama nchini . 2Mwenyekiti wa wakimbizi wa ndani walioathirika kufuatia ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 katika kaunti...