-Ni wakati wa kupokea habari za yard fm na AGR FM, abagusii global radio lakini kwanza tupate mkhutasari wake.
Naomba makanisa mjitolee tuombee nchi yetu -asema dakari Nyandoro
-Mbunge wa Nyaribari Masaba Elijah Moindi asema shule zizawadiwe baada ya kufanya vyema katika mitihani
-Wakaazi wa kisii waombwa kumpa gavana ongwae mda kufanya maendeleo.
-Wanaochimba barabara wakamatwe na kushtakiwa asema mbunge Timothy Bosire
HABARI KAMILI:
HABARI KAMILI:
1 Makanisa yote yameombwa kuombea nchi ya Kenya ili kuwe na amani na kuzuia visa vya mashambulizi kuendelea kushuhudiwa nchini.
Akiongea jana katika hafla ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa ya kiadventista ya Tindereti iliyoko eneo bunge la Borabu kaunti ya Nyamira daktari Yobesh Kambi aliomba wahumini wa makanisa mbalimbali kuendelea kuombea nchi ya Kenya ili amani iendelee kushuhudiwa.
Wakati uo huo, daktari Nyandoro aliomba wakaazi kushirikiana pamoja kuleta maendeleo katika jamii ya mkisii haswa katika kaunti ya Nyamira.
Hii ni baada ya kaunti ya Nyamira kusemekana kuwa imerudi nyuma kimaendeleo jambo ambalo viongonzi wengi kutoka kaunti hiyo hawajafurahishwa nalo huku viongonzi wengi wakshtumu uongonzi ulioko katika kaunti hiyo .
2 Mwanafunzi mmoja wa umri wa miaka 17 katika shule ya upili ya Mariindi iliyoko kaunti ya Nyamira kwa jina Judy Maasi amejitoa uhai wake baada ya kujirusha ndani ya choo ya shule hiyo yenye futi 60 leo asubuhi.
Akitibithisha kisa hicho OCPD wa kaunti ya Nyamira Ricah Ongare alisema mwanafunzi huyo aliyekuwa kidato cha tatu katika shule hiyo ya Mariindi alijirusha ndani ya choo leo mwendo wa saa 6:00 asubuhi baada ya kupatikna akiwa katika bweni ya shule hiyo akiongea na simu usiku wa kuamkia leo jambo ambalo ni kinyume na sheria za shule hiyo.
Inasemekana msichana huyo aliamua kujitoa uhai kwa kuogopa kuwa angechukuliwa hatua kwani alipatikana akiongea na simu usiku wa kuamkia leo na mwalim mmoja wa shule hiyo anayesimamia wanafunzi ambao wanaishi katika mabweni ya shule hiyo.
Mwili wa marehemu huyo umetolewa kwa choo hiyo na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Nyamira.
3 Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Masaba kaunti ya Kisii Elijah Moindi amesema shule ambazo zitafanya vyema katika mitihani ya kitaifa kutoka eneo bunge lake atazizawadi kama njia mojawapo ya kuwatia motisha walimu pamoja na wanafunzi.
Akizungumza jana katika eneo bunge lake mbunge huyo alisema shule zote ambazo zitafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa atahakikisha zimezawadiwa kati ya walimu pamoja na wanafunzi kama njia mojawapo ya kuinua viwango vya elimu juu zaidi katika eneo bunge lake.
Aidha mbunge huyo alisema baada ya shule ya upili ya wasichana ya St Charles Ichuni Lwanga amboyo iko katika bunge lake na ambayo iliweza kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana siku ya jumatatu ataikabidhi shule hiyo gari [school bus] ili iwe funzo kwa shule zingine kutia motisha.
Shule hiyo ya wasichana kutoka bunge lake ilifanya vizuri na kuorodheshwa miongoni mwa shule ambazo ziliweza kufanya vizuri katika kaunti ya kisii.
4 Mbunge wa Kitutu Chache kaskazini kaunti ya Kisii Jimmy Angwenyi amewaomba wakaazi wa kaunti ya Kisii kumpa gavana wa kaunti hiyo James Ongwae mda zaidi ili kutimiza miradi aliyo nayo kwa kaunti yake.
Akizungumza katika uga wa shule ya upili ya wasichana ya Marani iliyoko eneo bunge lake wakati wa hafla ya mazishi ya mfanyikazi wa mbunge huyo, mbunge huyo alisema kuna haja ya wakaazi kumpa gavana wakati mwafaka kutimiza miradi aliyo nayo katika kaunti ya Kisii
Wakati huo huo, viongonzi waliohudhuria hafla hiyo kutoka kaunti ya Kisii walihapa kufanya kazi pamoja ili viwango vya maendeleo kuinuka zaidi.
Viongonzi waliohudhuria hafla hiyo ni gavana Ongwae, mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyonka, Seneta mteule kaunti ya Kisii Hosea Onchwang’i, wawakilishi wa wadi mbalimbali za kaunti ya Kisii pamoja na wananchi wote kwa jumla.
5 Mbunge wa eneo Bunge la Kitutu Masaba, Kaunti ya Nyamira Timothy Bosire amewaomba Askari wa utawala na Machifu kufanya uchungunzi kuhusu wale wana tabia ya kulima na kupanda mgomba wa ndizi kwenye barabara za eneo bunge hilo.
Akiongea katika shule ya upili ya Rigomba iliyoko eneo bunge lake iliyochomeka mwenzi moja uliopita na kuifadhili Sh900,000 ili kujenga bweni mpya, Mbunge Bosire aliwaomba Askari pamoja na machifu kuwakamata na kuchukuliwa hatua za Kisheria wanaochimba barabara wakidai ni njia moja ya kulalamikia barabara mbovu.
Wakati uo huo, Mbunge huyo aliwakosoa vikali wale wanafanya uharibifu huo wa barabara na kusema ni kukiuka sheria za nchi ya Kenya
6 Wakaazi wa kaunti ya Kisii wamehimizwa kupanda miti kama njia moja ya kutunza mazingira huku wakishauriwa kuhakikisha kuna usafi kila mahali ili kuepukana na mkurupuko wa magonjwa kama vile kipindupindu.
Akiongea katika shule ya msingi ya Kisii wakati wa kuadhimisha siku ya mzingira ulimwenguni, msimamizi wa mkahawa wa Ufanisi Isabellah Lumumba alisema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa ametunza mazingira.
Lumumba pia aliiomba serikali ya kaunti ya Kisii kuwa katika msitari wa mbele katika upanzi na uhifadhi wa mazingira,
Lumumba aliihimiza kuelimishwa kwa watoto kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ili wanapokuwa wawe wanafahamu maana ya uhifadhi wa mazingira.
Comments
Post a Comment