Skip to main content

Taarifa ya 06/11/2015

1]Mwenyekiti wa wakimbizi wa ndani walioathirika kufuatia ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 katika katika kaunti za Nyamira na Kisii ameomba serikali kuu kuwachukulia hatua kali ya kisheria wale wanajitambulisha kuwa wakimbizi ili kufadhiliwa na serikali.

Akiongea siku ya Jumatano na waandishi wa habari katika uwanja wa michezo wa Gusii, mwenyekiti huyo Nemuel Momanyi alisema kuna baadhi ya watu ambao wanajitambulisha kuwa wakimbizi wa ndani ilhali hawakufurushwa kutoka popote ila ni mbinu ya kufadhiliwa na serikali ya kitaifa.
Hii ni baada ya wakimbizi wa ndani 23,000 katika eneo la Gusii wanaostahili kufadhiliwa na serikali kusema kuwa hawajawahi pata msaada wowote kutoka kwa serikali hadi sasa.
 Wakati huo huo mwenyekiti huyo alisema kuwa ni wakimbizi hao bandia wanaishi vizuri baada ya kupata pesa za bure kutoka kwa serikali ilihali wale halisi wanasumbuka.

2] Mbunge wa Homa-Bay Town Peter Kaluma ameziomba Serikali za ugatuzi pamoja na ile ya kitaifa kushirikiana pamoja na kufanya maendeleo katika sehemu zote nchini.

Akizungumza siku ya Jumanne katika ukumbi wa Gusii Cultural Hall mjini Kisii kwenye hafla ya kusanya maoni ya wanchi kuhusu pesa za hazina ustawi maeneo bunge (CDF), Mbunge Kaluma alisema sharti Serikali za ugatuzi na ile ya Kitaifa zishirikiane ili kufanya maendeleo zaidi katika sehemu zote za nchi.
Matamshi ya mbunge huyo yaliungwa mkono na Mbunge wa Nyaribari Masaba Elijah Moindi ambaye alisema kuwa Serikali zote zikishirikiana pamoja maendeleo yatafanyika zaidi katika sehemu za mashinani huku akiomba viongonzi wote kuweka siasa kando na kutilia maanani maendeleo. 
hospitalli moja. [Picha/ Money-kisumunews.com]]

3]Mwanasiasa mmoja kutoka eneo bunge la Nyaribari Chache katika kaunti ya Kisii Rael Otundo amesema pesa ambazo serikali ya kaunti ya Kisii ilitenga kuwanunulia wananchi kadi za matibabu ya NHIF zinastahili kutumika kununua dawa katika hospitali moja ili kuwafaidi Wananchi wote.
Akizungumza siku ya Jumanne katika hafla ya mazishi katika kijiji cha Nyanguru, kaunti ya Kisii, mwanasiasa huyo alisema ununuzi wa kadi hizo za NHIF hautasaidia maanake si kila mtu atafaidi.
Hii ni baada ya gharama ya kuilipia kadi hiyo kupanda kutoka shillingi 160 hadi shillingi 500 kwa kila mwezi, ambazo serikali ya kaunti ya Kisii haitaweza kulipa kila mwaka maana zitakuwa nyingi na kuigharimu serikali kutumia pesa nyingi zaidi.

4]Mbunge wa Nyaribari Masaba, Kaunti ya Kisii Elijah Moindi amewaomba wakaazi wa kaunti hiyo kuchukua hatua kwa Wabunge wanaoshukiwa kutumia vibaya pesa za hazina ya CDF.

Akiongea siku ya Jumanne katika ukumbi wa Cultural Hall mjini Kisii wakati wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu hazina ya CDF kusalia kuwa katika Serikali ya Kitaifa au iwe chini ya Serikali za kaunti, Mbunge Moindi aliomba wakaazi hao kuwashtaki  Wabunge ambao wanatumia pesa za maendeleo ya CDF vibaya ikiwa wana ushahidi wa kutosha.
Wakati uo huo, Mbunge huyo aliomba wananchi kuunga mkono maendeleo yanayofanywa katika maeneo bunge yao kupitia pesa hizo za CDF ili maendeo yainuke zaidi katika Kaunti ya Kisii.
Kwa upande mwingine viongozi waliohudhuria hafla hiyo waliunga mkono pesa hizo kubaki kwa Serikali ya kitaifa na ziongezwe zaidi kutoka asilimia 2.5 hadi asilimia 10.

5]Mwili wa mwanaume wa miaka ishirini na tisa ulipatikana ukiwa kando mwa mto Iyenga katika wadi ya Gesusu Kaunti ya Kisii Jumanne asubuhi.

Mwanamme huyo alitoweka kutoka kwake kwa njia isiyo eleweka siku tatu zilizopita, na kisha mwili wake kupatikana ukiwa kando mwa mto huo ulio eneo la Raganga, katika wadi ya Gesusu.
Inasemekana mwenda zake alitoka kwake na wenziye, lakini hakuregea jioni, huku mke wake akiripoti kwa ndugu zake na wakaanza shughli za kumsaka siku iliyofuata, na juhudi zao zilikumbwa na changamoto kwani hakuwa na simu.
Walipiga ripoti kwa chifu wa eneo hilo Bw Machogo Nyauma, ambaye pia alichukua hatua siku ya tatu kumtafuta bila mafanikio na kisha baadaye, mnamo saa tatu asubuhi wapita njia wakamtambua akiwa amefariki.
Mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha Gucha Keroka, katika Kaunti ya Kisii, huku hicho kikiendelea kufanyiwa uchunguzi.
Chifu huyo aidha alisema amewaarifu polisi ambao wameanza kuchunguza kisa hicho ambacho ni cha aina yake

Na katika Michezo

Timu ya Shabana inayoshiriki ligi ya FKF inaendelea na mazoezi katika uga unaokarabatiwa wa Gusii, ili kujiandaa kwa mechi yao ya siku ya Jumapili dhidi ya FC Talanta.

Mechi hiyo ambayo itachezewa katika uwanja wa Awendo Green mjini Awendo, itashuhudia vijana hao wa Kisii wakikwaruzana na vijana wa Talanta, kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kuwa ngumu.
Shabana, chini ya ukufunzi wa James Nandwa inashikilia nafasi ya kumi na moja kwenye jedwali la ligi ya FKF, na itakuwa ikijiandaa kuhakikisha matokeo yao yanaimarika.
Aidha, timu hiyo imekumbwa na habari mbaya, kufuatia fununu kwamba mchezaji wa kiungo cha kati Sunday Mutuku atahama klabu hiyo baada ya kandarasi yake kukamillika.
Mutuku, ambaye ameisaidia sana timu hiyo ameonyesha nia ya kuhama timu hiyo, huku fununu zikionyesha kuwa huenda akajiunga na Muhoroni Youth ingawaje habari hizo hazijadhibitishwa.
Kocha Nandwa amesema hatima ya Mutuku itajulikana pindi tu akapozungumza naye.
Halikadhalika, kocha huyo amesema kwamba bado timu hiyo ina nafasi nzuri ya kutua ubingwa wa ligi ya FKF, ikiwa watajizatiti na kutia bidii mara dufu

Hizi ndizo habari zetu zikitanyarishwa kwenu na Brighton Makori na kusomwa na Orina Ontiri

Comments

Popular posts from this blog

Police: Girl, 7, Survives Ky. Plane Crash; Police ID 4 Dead

 A 7-year-old girl survived a plane crash in Kentucky that killed four people Friday night, and the disoriented little girl walked away from the wreckage and reported the crash to a local resident, authorities said. The small Piper PA-34 reported engine trouble and lost contact with air traffic controllers as it was flying over the southwestern part of Kentucky about 5:55 p.m. CST, the FAA said. About a half hour later, a Lyon County resident called 911 and told dispatchers that a 7-year-old girl had walked to his home and said she had been involved in a plane crash, said Sgt. Dean Patterson of the Kentucky State Police. "This girl came out of the wreckage herself and found the closest residence and reported the plane crash," Patterson said. "It's a miracle in a sense that she survived it, but it's tragic that four others didn't." The girl was in emotional distress and taken to a hospital with non-life-threatening injuries, Patterson said. At th...

Kisii Senator Chris Obure and three former Permanent Secretaries charged over corruption related to the multi-billion shilling Anglo Leasing scandal.

Kisii Senator Chris Obure and three former Permanent Secretaries were on Wednesday charged over corruption related to the multi-billion shilling Anglo Leasing scandal. Obure who was charged over crimes committed when he was a Minister of Finance in former President Daniel arap Moi’s government, was in the dock alongside former Transport and Communication Permanent Secretary Sammy Kyungu, former PS Ministry of Finance Joseph Magari and former PS for Internal Security and Provisional Administration Dave Mwangi. They have all denied abuse of office and conspiracy to commit economic crime charges, although Mwiraria and the Kamani’s who are represented by lawyer Ahmednassir Abdullahi were not in court/CFM NEWS Also charged alongside them were former Postmaster General Francis Chahonyo, former Finance Secretary Samuel Bundotich and David Onyonka who was in-charge of debt management in the Ministry of Finance at the time he is accused of committing economic crimes. David Mwiraria who...

Boinett koegwa amatuko emerongo etano nomo komobwata Lengoboini

Ekegambero ekenene kia Nakuru kiamoeire omonene bwa abanyanyimbo omogeni omosike Joseph Boinett amatuko emerongo etano nomo komobeka biara omoriki bw' ekeombe kia abaorokia gia TSC nyumba yogosinywa goakana abaorokia baria batimokire korwa emeremo goakanwa. nigo gekobooria buna abekwe chingayo emetienyi etano nomo emegima ase ogosinywa kobaakana chibillion 16.7 chia aboorokia ang'e 56,000. Rero omokonyi o Inspector General Samuel Arachi nigo aoroka bosio bwa Justice Janet Mulwa koorokia buna ninki gekogera okobwatwa kwa Lengoiboini gwachigetwe omotienyi o kabere chitariki emerongo ebere gotaraikeranigwa na abanyanyimbo.Arachi nigo agoteba abeire abisi ase emeremo ebetereretie chingaki ogochika owko kwarwetwe chitariki 26,na akamanyigwa ekero airanete chitariki isato omotienyi o gatato. Nigo boigo amentire buna onorai oyio nigo abeire isiko y'ense gochakera chitariki 28 omotienyi o kabere koirera okoegwa riuko erio koba egento egekong'u pa.