--Waziri wa fedha Henry Rotich asoma Bujeti ya mwaka wa 2015-2016 .
--tunaomba serikali kuwatia mbaroni wakimbizi ghushi asema mwenyekiti Nemuel Momanyi
--ni haki yetu hatutarudisha sare za kazi wafanyikazi wa nyamira wasimama kidete.
--kamishena wa kisii chege mwangi kuzuru eneo la gesure hivi karibuni
1 Bajeti ya mwaka wa 2015-2016 imesomwa hii leo katika ukumbi wa bunge la kitaifa ikiwasilishwa na waziri wa fedha nchini Henry Rotich.
Bajeti hiyo ya pesa taslimu shillingi trillion mbili itanufaisha baadhi ya sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kutengeneza barabara kutengewa kiwango kikubwa cha pesa.
Hii ni mara ya pili bajeti kusomwa chini ya uongonzi wa serikali ya Jubilee huku wakenya wengi walikuwa wanatarajia bei ya bidhaa kushuka na hata masuala muhimu ikiwa suala la kuimarisha usalama nchini .
2Mwenyekiti wa wakimbizi wa ndani walioathirika kufuatia ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 katika kaunti za Nyamira na Kisii ameomba serikali kuu kuwachukulia hatua kali ya kisheria wale wanajitambulisha kuwa wakimbizi ili kufadhiliwa na serikali.
Akiongea hiyo jana na waandishi wa habari katika uwanja wa michezo wa Gusii, mwenyekiti huyo Nemuel Momanyi alisema kuna baadhi ya watu ambao wanajitambulisha kuwa wakimbizi wa ndani ilhali hawakufurushwa kutoka popote ila ni mbinu ya kufadhiliwa na serikali ya kitaifa.
Hii ni baada ya wakimbizi wa ndani 23,000 katika eneo la Gusii wanaostahili kufadhiliwa na serikali kusema kuwa hawajawahi pata msaada wowote kutoka kwa serikali hadi sasa.
Wakati huo huo mwenyekiti huyo alisema kuwa ni wakimbizi hao bandia wanaishi vizuri baada ya kupata pesa za bure kutoka kwa serikali ilihali wale halisi wananasumbuka.
3 Mwathiriwa mmoja wa ghazia za uchaguzi wa mwaka wa 2007-2008 ameiomba serikali kumsaidia ili kujiendeleza kimaisha.
Akiongea na Waandishi wa habari hiyo jana katika hafla ya wakimbizi wanaotafuta haki ya kusaidiwa na Serikali katika uwanja wa Gusii, mwathiriwa Simeon Atandi Monyancha kutoka Bomorenda, eneo Bunge la Bonchari katika Kaunti Ya Kisii alielezea shida alizokumbana nazo katika mwaka wa 2007 wakati alikatwa mikono yake wakati wa ghazia za uchaguzi wa 2007-2008 katika sehemu ya Sotik.
Monyancha aliyekuwa na huzuni mwingi akiyasema aliyokumbana nayo wakati huo kwa sasa anaiomba Serikali kumsaidia kuweza kujipatia mapato ya kila siku.
Monyancha ambaye ni baba ya watoto sita na wake wawili, ilhali mkewe wa kwanza aliaga, alisema kuwa ana kibarua kigumu ya kulisha familia yake kwani hana lolote afanyalo kwa kukosa mikono yake miwili.
Monyancha alisema kuwa alikuwa akifanya kazi ya kuchuna majani chai alipokumbana na kisa hicho kilichomwacha bila mikono kwani alikatwa mikono na wenye walikuwa na maoni tofauti ya kisiasa.
4Askari wa Kaunti ya Nyamira waliosimamishwa kazi wamelipinga ombi la Serikali ya Kaunti hiyo kuwahitaji kuzirudisha sare zao za kazi walizopewa hapo mbeleni.
Wakizungumza na Wandishi wa habari hiyo jana katika mji wa Nyamira, wafanyikazi hao sasa wanataka haki itendeke kwa kupata suluhu mwafaka unaozingira kesi yao.
Mkuu wa Idara ya fedha katika Kaunti ya Nyamira John Omanwa amekanusha madai hayo ya kusema wanakandarasi walioajiriwa na Serikali ya kaunti hiyo ya Nyamira wamefutwa kazi ila wamesimamishwa kazi kufuatia wakati wao waliopatiwa kufanya kazi kama wanakandarasi kufika mwisho.
Aidha, Omanwa alisema watu huajiriwa katika kaunti hiyo kwa muda kati ya miezi mitatu hadi sita na watu hao pia kutafute ajira upya kufuatia sheria za Serikali ya kaunti hiyo.
Askari hao hata hivyo wamesimama kidete kwa kusema hawatarudisha sare zao ila kutendewa haki kama wakaazi wa kaunti hiyo.
5 Kamishena wa kaunti ya Kisii Chege Mwangi amewahakikishia wakaazi wa kata ndogo ya Gesure wilayani Sameta kaunti ya Kisii kuwa atazuru katika sehemu hizo kutafuta suluhu la kulalamikia kuajiriwa kwa naibu chifu wa eneo hilo ambaye anasemekana hakuajiriwa kwa njia ya haki ila ni kufuata ukoo wa nyumba Fulani.
Alizungumza afisini mwake hiyo jana kamishena Chege Mwangi alisema atazuru sehemu hizo hivi karibuni kutatua malalamishi ya wakaazi wa eneo hilo .
Hii ni baada ya yakaazi wa eneo hilo la Gesure kuandamana hadi ofisi yake hiyo jana wakiongozwa na David Ogega wakilalamikia kuajiriwa kwa naibu chifu wa lokesheni hiyo ya Gesure huku wakisema ni ufisadi na anatoka ukoo mmoja na chifu wa eneo hilo wakisema ni ufisadi kwa wakaazi wengine.
Sasa ni rasmi kuwa kamishena amesikia kilio chao na kuwahakikishia wakaazi hao kuwa atazuru sehemu hizo ili kusuluhisha mambo hayo.
Habari ambazo zimeandaliwa na Denis zadock na Brighton makori
Comments
Post a Comment