Skip to main content

TAARIFA LEO 06/10/2015

Hizi ni habari zetu sikitayarishwa na Peter Onkoba na Brighton makori 10th  June 2015

1]Hafla ya kukusanya maoni kutoka kwa wakaazi wa Kisii ambayo ilifanyika jana Jumanne katika ukumbi wa Cultural Centre ilishuhudia watu wachache sana ambao walihudhuria kongamano hilo.

Kampeni hiyo ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda sasa kwenye kaunti mbali mbali kote nchini, iliweza kuhudhuriwa naye mwenyekiti wa pesa za maendeleo za maeneo bunge maarufu kama CDF, Elias Mbao pamoja na mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Masaba  Elijah Moindi ambaye pia ni mwanachama wa kamati teule ya bunge inashughulikia pesa hizo za CDF ambaye pia anawakilisha kaunti mbili za eneo la Gusii; Kisii na Nyamira.

Ukumbi huo ambao kwa kawaida hujaa pomoni kunapokuwa na hafla kama hizo, ulijazwa nusu, ambapo mwenyekiti Mbao alivilaumu vyombo vilivyowajibishwa kusambaza ujumbe huo kwa kutofanya kazi yao kikamilifu.

Hata hivyo, wengi waliohudhuria kongamano hilo waliunga mkono kuwe na pesa hizo za maendeleo ya maneo bunge, ila wakapendekeza kubadilishwe watu na wasimamizi ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano na wabunge wa maeneo ya uwakilishi.

Hafla hiyo ya kukusanya maoni imekuwa ikikusanya maoni kutoka kwa kaunti tatu katika kila kikao, ambapo hafla ya leo iliweza kuwakutanisha wakaazi wa kaunti za Kisii, Nyamira pamoja na kaunti ya Migori.

 2]Senate wa kaunti ya Nyamira amemtaka gavana wa kaunti hiyo kuhakikisha wafanyakazi wa vibarua wanalipwa pesa zao.

Senata huyo pia amewataka wafanyikazi hao kupewa kipaumbele katika kazi ambazo zimetangazwa na kaunti hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari katika mji wa Nyamira siku ya Jumatatu, Seneta Okong’o Mong’are alishangazwa na swala hilo la kaunti hiyo kutowalipa wafanyakazi hao wa vibarua.

Alisema kuwa kuna pesa zilizotengwa kushughulikia malipo ya wahudumu wote wa kaunti ambao hufanya kazi katika vitengo mbali mbali katika kaunti hiyo.

Mong’are alimtaka gavana wa kaunti ya hiyo, John Nyagarama kuwajibikia maswala yanayomlenga.

Alimtaka gavana kushughulikia swala hilo liloripotiwa katika vyombo vya habari kuhusiana na vibarua ambao wanahudumu katika hospitali ya Nyamira level five ambao wamekuwa wakilalamikia kutolipwa hela zao kwa muda sasa.

Seneta huyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa gavana wa kaunti hiyo yake kwa siku za hivi karibuni.

3Mbunge wa Homabay Town amewataka viongozi wote kutoka eneo pana la Nyanza Kusini ikiwemo Kisii kuunga mkono pesa za maendeleo ya maeneo bunge CDF, ili zibaki katika mikono ya wabunge.

Akiongea hiyo jana Jumanne  kwenye hafla ya kukusanya maoni kutoka kwa wakaazi wa kaunti za Kisii, Migori na Nyamira ambayo ilifanyiwa kwenye ukumbi wa umma wa Cultural Centre, Kaluma alisisitiza umuhimu wa pesa hizo ambazo alisema kuwa zimesaidia pakubwa kwa kuinua maendeleo ya maeneo ya mashinani.

Aliahidi kupigana hadi mwisho kuhakikisha pesa hizo zinabaki chini ya mamlaka ya wabunge, na kuona kuwa zinasimamiwa vizuri na pia kudokeza kuwa atasimamia mswada ambao utahakikisha kuwa matapeli ambao wamekuwa wakiwekwa na viongozi flani kusimamia pesa hizo wanaondolewa ili kulisafisha jina la usimamizi wa pesa hizo.

Pesa za maendeleo ya maeneo bunge zimekuwa na mzozo kati ya maseneta na magavana, huku wengi wa wananchi na viongozi wakitaka sheria maalumu kuwekwa ili kutoa uangalizi na usimamizi ulio wazi wa fedha hizo ambazo licha ya kufanya maendeleo katika mashinani, zimelaumiwa kwa kutoa mwanya kwa wabunge wengi kuwa wafisadi na kuwaajiri jamaa zao kusimamia miradi inayofadhiliwa na hela hizo.

Na katika Michezo

4Katibu mkuu wa michezo ya riadha katika viwango vya shule za msingi katika eneo la ziwa kuu Ben Ochieng’, amesema kuwa na imani wataibuka na ushindi mkubwa katika mashindano ambayo yalimalizika juzi  Jumatatu katika chuo cha Kisii.

Ochieng’ alikuwa akitoa hutuba yake ya kufunga mashindano hayo yaliyozikutanisha shule zaidi ya 30  za msingi kutoka kaunti za Migori, Homabay, Siaya, Kisumu, Nyamira pamoja na mwenyeji kaunti ya Kisii, ambapo hakuficha furaha yake kufuatia hali njema ya anga ambayo iliwapa nafasi mwafaka ya kufanikisha mashindano hayo bila shida.

Hata hivyo, katibu huyo alionyesha wasiwasi wake kwa wapinzani kutoka maeneo ya Bonde la Ufa ambalo alisema limekuwa mpinzani mkubwa, na kuwataka washiriki wote kuendelea kujiandaa mapema ili kuboresha matokeo hayo kufikia wiki ijayo tarehe 12 kutakapofanywa mashindano ya kitaifa.
Ochieng’ hakusita kuwaomba wanafunzi walioteuliwa kutumia faida ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa kuibuka na ushindi mnono.

Bado mashindano hayo hayajaamuliwa ni wapi hasa yataandaliwa kati ya uga wa michezo wa Gusii na ule wa chuo Kikuu cha Kisii, lakini Ochieng’ aliweza kudokeza kwamba huenda wakatumia uga wa Gusii kufuatia gavana wa kaunti hiyo kusema kuwa Chuo cha Kisii huenda kuwe na hafla nyingine.Mashindano hayo yataanza tena hapo kesho yakijumuisha kaunti zote.

5]Mwanafunzi wa miaka 11 alishangaza watazamaji waliojumuika katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Kisii siku ya Jumatatu baada ya kumenyana na zaidi ya wapinzani 50 kwenye mbio za mita 10,000 na kuibuka nambari tatu.

Mwanafunzi huyo alifuzu kuingia katika kikosi kitakachowakilisha eneo la ziwa kuu kwenye michuano ya riadha ya kitaifa ambayo itafanyika wiki ijayo.

Mwanafunzi huyo, Jane Ghati kutoka shule ya msingi ya Nyabikongori katika Kaunti ya Migori, alipata upinzani mkubwa kutoka kwa wanafunzi wenzake ambao walionekana kuwa na miili mikubwa na kuwa na misuli iliyotutumka lakini mtoto huyo hakushtushwa na wenzake hadi ilipofika mzunguko wa mwisho alitoka nambari ya kama kumi na tano ambapo aliwapita wanariadha waliokuwa mbele yake na kuridhika na nambari tatu.

Akiongea nawatangazaji wetu  baada ya kukamilisha shindano hilo, Ghati alionyesha furaha kubwa kwa kuteuliwa kuwakilisha eneo la Nyanza na kusema kuwa atajitahidi ili kufanya vizuri zaidi na kushinda wenzake katika kitengo hicho.

Mwenyekiti wa riadha kutoka kwenye kaunti anakotokea mwanafunzi huyo John Samwa, alisikitikia ukosefu wa msaada wa kifedha kutoka kwenye kaunti yao ya Migori, hali ambayo alitaja kuwa chanzo cha kuwasafirisha wanafunzi wachache kuwakilisha kaunti hiyo katika mashindano hayo.

Lakini mwenyekiti huyo hata hivyo alionyesha moyo wa kumpa motisha mwanafunzi Ghati kutimiza ndoto yake ya kuafikia mafanikio kwenye mbio hizo za mita 10,000.

                                           Thanks by Yard Family

Comments

Popular posts from this blog

ICC: Abasoeri na abaegereri komogorerana ekegambero ekenene kia ICC

Ekeombe kia obosoeri aaria chinsemo chia ICC nigo bamogorerana rituko ria rero ase okogenderera kobora gwa kirori P0727. Koreng'ana na obosoeri, kirori oyio noyobengencho enene. Korwa abakweegerera Ruto na Sang', nigo baangire kirori oyioo taganywa ekiagera babakoreire chimgaki na ebiro gose koegwa ribaga ria bene komoringooria orogendo rwaye oborori bwaye botarategererwa. Nigo ekageire buna kirori oyio nere oyo' omoerio. Ankio nigo ekegambero kerarwe ribaga ase ebiombe ebio bibere kogayana ogotaigwana okwo.

Dallas/Ft. Worth hit with up to 7 inches snow!

It’s a winter wonderland in Dallas/Ft. Worth! We were expecting the sleet and freezing rain last night but the snow was an added bonus! Between 3 and 7 inches dropped across the metroplex. Temps are expected to get up to around 37 which means some of ice and snow will melt but temps will drop below freezing tonight causing what melts to re-freeze-KRNB

Hey Men.....6 Ways Men are Destroying their Sperm

It’s not only women who suffer from infertility problems. Men are also the victim to fertility issues. The sperm plays an important role in fertilization. The lifestyle people lead today lead to the disintegration of the quality of the sperm and its production. Here are some issues that affect his sperm levels: Keeping their phones in the front trouser pockets All of us know the ill effects of radiation emitted from our phones and yet we choose to keep them in our trouser or jeans pockets. It’s not all talk but research that has proved that the radiation emitted from our phones kill the sperms in his pants. So if you are worried about fertility issues, remind your guy to keep his cellphone elsewhere. Excessive smoking Smoking is bad for the overall health. It even affects the sperm in a negative way. Smoking apart from reducing the  sperm count  also prevents it from moving around. Stress Stress affects all our bodily functions including the production o...