Skip to main content

Bwana Yesu Kristo hakufa Msalabani ili atimize Ndoto Yako

LUGHA MPYA: Mtazamo wa ulimwengu, nia ya kibinadamu na ya wasioamini zimeingia fikra za waumini wengi sana.

Wapendwa wasomaji, wapi katika Agano Jipya  tunasoma kwamba Yesu au mitume wanawasisitiza waumini wazifuate ‘ndoto’ zao? Haipo! Wapi katika maandiko ya Biblia  waandishi wanatumia lugha ya ‘zifuate ndoto zako’? Haipo! Wapi Bwana Yesu alisema, “Nimekuja kuitumiza ndoto yangu.”? Haiwezekani! Siyo ndiyo? Yesu wala mitume wake hawakuitumia lugha hiyo au maneno haya! Wazo hili linapinga mafundisho ya neno la Mungu. Wazo hili linainua hamu yangu yenyewe au tamani yangu ya binafsi kuliko mapenzi ya Mungu kwa maisha yangu! Ni mafundisho ya hatari sana siku hizi.

Bwana Yesu hakufa ili atimize ndoto yako bali mapenzi ya Mungu yatimizwe katika maisha yako.

Watu, na hata wahubiri, wanasema, ‘Fuata ndoto zako!’ Lakini Yesu alisema, ‘Nifuate mimi’. Ikiwa utafuata ndoto zako, unajifurahisha mwenyewe tu. Lakini ikiwa utamfuata Yesu, atampendeza Yeye. Kama utafuata ndoto zako, basi unajitumikia wewe mwenyewe. Ukimfuata Yesu, utamtumikia Yeye na kanisa lake. Kama utafuata ndoto zako, unajitengenezea njia yako mwenyewe. Kama utamfuata Yesu, Yeye ndiye atakayekuandalia njia. Kama utajitahidi kutimiza ndoto zako au mtazamo wako, utakosa mapenzi ya Mungu; kama ‘utatoa mwili wako uwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu na hutaifuatisha namna ya dunia hii, bali kugeuzwa kwa kufanywa upya nia zako, ndipo utakapojua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza na ukamilifu.’

Watu wengi siku hizi wanafuata ‘ndoto’ zao au wanajitahidi kuutengeneza ‘mtazamo’ wao ili ‘wafanikiwe’ wakati wakidai au wakifikiri hiyo ni sawasawa na mapenzi ya Mungu, lakini wanajidanganya au wanaruhusu mhubiri fulani kuwadanganya. Yesu hakuifuata ndoto yake – hiyo ni kinyume cha tabia Yake! Kinyume cha wazo hili la siki hizi Yesu alisema, “Kwa kuwa mimi SIKUSHUKA kutoka mbinguni ILI NIYAFANYE MAPENZI YANGU, bali MAPENZI YAKE aliyenipeleka.” (Yoh.6:38). Huo ulikuwa msingi wa maisha ya Mwana wa Mungu! Na kama wakristo tunapaswa tuwe na msingi ule ule! Kumbe, kwa maneno machache Bwana Yesu amebomoa ndoto nyingi ya waumini ya siku hizi, ameharibu mafundisho haya ya udanganyifu! Je, ndoto yako ni sawasawa na mapenzi ya Mungu kwa maisha yako? Unajuaje? Kwa wengi, chakula chao ni kuota ndoto wafanikiwe, au wawe kitu, kama mwimbaji, mwenye biashara, au mpiga gitaa – wanajisikia kiu sana kwa ajili ya tekelezo la ‘ndoto’ zao au ‘mtazamo’ wao! Kinyume chake neno la Mungu lilimjia Baruku, “Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo.” (Yeremia 45:5).

Yesu alisema, “Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi YAKE aliyenipeleka, nikaimalize kazi YAKE.” Na wewe? Unafuata ndoto yako au unaifuata njia ya Yesu Kristo – yaani, hufuati mapenzi yako bali mapenzi ya Mungu? Udanganyifu ya siku hizi ni kwamba watu wanachanganyika kabisa kabisa ‘ndoto yangu’ na ‘mapenzi ya Mungu kwa maisha yangu.’ Bila kusoma Biblia, bila kuamini Biblia, bila kufiri hata kidogo juu ya yale Biblia isemayo, watu wanasawasisha ‘ndoto yangu’ na ‘mapenzi ya Mungu’ na wanaandika maneno bila maana kabisa kama, “Usikate tamaa. Mungu atatimiza ndoto yako” au “bila ndoto hutapata cho chote!” Watu hawa hawajali neno la Mungu, wanapuuza mafundisho ya Biblia, wanatangaza maneno matupu!

Na hapo tunakutana na udanganyifu ya mafundisho hayo; yaani, wahubiri hawafuati neno la Mungu bali badala yake wanachochea HAMU YA BINAFSI ya watu, TAMANI YA WATU WENYEWE wawe kitu au kuwa na kitu. Kwa mafundisho yao wanaacha lugha ya Biblia, wanaondoa wazo la ‘mapenzi ya Mungu’ na badala yake wanatumia neno ‘ndoto’ na wanasawasisha hamu ya binfasi ya mtu na mapenzi ya Mungu, yaani, hawatofautishiani kati ya ‘ndoto yangu’ na ‘mapenzi ya Mungu’. Matokeo ya mafundisho haya na lugha hiyo ni machanganyiko na udanganyifu. Ni wazi watu watafurahi kusikia mambo haya. Kwa nini? Kwa sababu sasa hamu yangu – kwa mfano niwe mwimbaji – inawakilisha ‘mapenzi ya Mungu’ kwa maisha yangu! Vijana wengi ulimwenguni wanataka kuwa mwimbaji, na sasa waumini wengi wa viajna wanataka kuwe waimbaji au wapiga gitaa. Kwa wengi – wakiwa wasioamini au waumini – hili ni jambo la kujipendeza tu! Linatokana na tabia ya kibinadamu tu. Kwa wengi hiyo siyo mapenzi ya Mungu, lakini kutokana na mafundisho hayo ya udanganyifu, watu hawa wengi sasa wanafikiri lazima Mungu atatimiza tamani yao wawe kitu kwa sababu ‘ndoto’ yao ni sawa na mapenzi ya Mungu! Kwa nini watu wanafurahia mafundisho haya? Kwa sababu yanaruhusu, na hata yanachochea tabia ya kujipendeza! “Ahhh. Ninayo shauku sana…niwe na recording studio…niwe na biashara…kuhamishwa kutoka katika mazingira yangu magumu…nkd.” Ndiyo, watu wanayo shauku kama hizi na labda siyo mbaya, lakini kutokana na mafundisho ya siku hizi, kumbe, ‘shauku’ yangu ya binafsi zimebadilika na sasa zinawakilisha mapenzi ya Mungu! Kumbe, sasa ‘njia’ ya Yesu inanipendeza kwa sababu ni njia kutimiza hamu yangu! Hapana! Ni udanganyifu! Yesu alitangaza kwa wazi kabisa, “Akawaambia WOTE, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na AJIKANE MWENYEWE, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate…. Kama mtu akija kwangu naye hamchukii …nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” (Luka 9:23, 14:26).

Ni siku za hatari sana. Vijana wengi wamedanganywa kufikiri ndoto zao au mitazamo yao zinawakilisha mapenzi ya Mungu, kwa hiyo…

Kwa wengi, ndoto zao hazitatimizwa.

Kwa wengine ndoto zao labda zitatimizwa lakini haimaanishi ni mapenzi ya Mungu kwa maisha yao! Inategemea kabisa!

Waumini wengine wanangojea ngojea matekelezo ya ndoto zao. Badala ya kufuata kwanza ufalme wa Mungu na haki Yake, akili zao zimejazwa na mawazo ya ndoto zao; badala ya kumpenda Yesu kwa mioyo yao yote, mioyo yao zimeshikwa na hamu zao kuona matekelezo ya ndoto zao; badala ya kuyatafuta mapenzi ya Mungu (ambayo inawezekana yatakatisha ndoto zao!), wao wanaongozwa na ndoto zao katika mawazo na matendo yao – wanajitoa kwa ndoto zao kuliko kwake Mungu. Lakini kwenye facebook au kwenye semina fulani wahubiri au waandishi watajaribu kuzimarisha ndoto zao kwa kuwatia moyo ili wasikate tamaa. Lakini ndoto zao hazitatimizwa kwa sababu hazijajengwa juu ya mwamba wa neno la Mungu bali juu ya mchanga wa mawazo ya ulimwengu na juu ya ‘tamani’ ya watu tu! Waumini wengi hao watashindwa kuona tekelezo la ndoto zao, na kwa hiyo watakata tamaa sana na inawezekana wengine wao wataacha imani, wataacha kumfuata Yesu. Ni jambo la kuhuzunishwa sana na ninaandika mambo haya ili hata kijana mmoja tu ageuke na kuacha udanganyifu huo.

Ninaandika mambo haya kwa sababu siku hizi wahubiri wengi kupitia mafundisho yao wanatayarisha kizazi hiki cha vijana kuanguka kwa sababu wanaacha kuhubiri msalaba wa Kristo na kutokana na hayo vijana hawana msingi wa msalaba wa Yesu Kristo katika maisha yao. Wanafundishwa kuishi maisha ya kujipendeza badala ya kujikana. “Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo.” (1 Tim.4:1).

Yesu Kristo hakufa msalabani ili kutimiza ndoto zako!

Siyo kazi yangu kuota ndoto kwa maisha yangu! Jukumu langu ni ‘kutoa mwili wangu uwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu na kugeuzwa kwa kufanywa upya nia yangu, ndipo nitakapojua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza na ukamilifu kwa maisha yangu.’ Jukumu langu ni ‘niufuate kwanza ufalme wa Mungu na haki Yake NA HAYO YOTE MTAZIDISHIWA! Bwana asifiwe sana! Sisi hatuwezi kukosa cho chote ambacho kinahusu mapenzi ya Mungu kwa maisha yetu kama tukifuata neno la Mungu! Ni rahisi. Hatuhitaji kwenda chuo kikuu kuelewa ukweli wa Mungu! Inatosha kabisa tuwe kama watoto wachanga (Matayo 11:25). Kama tukitoa maisha yetu yawe dhabihu iliyo hai, Mungu Mwenyewe atatimiza mapenzi yake katika maisha yetu kwa wakati Wake!

Usinelewe vibaya. Siyo kosa kuwa na hamu au lengo! Lakini lazima tuwe watumishi wa Bwana na kufuata neno lake lisemalo, “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.” (Mithali 3:5,6). Mtumaini Bwana na siyo ndoto yako! Usizitegemee ndoto zako bali mtegemee Mungu! Katika njia zako zote usikiri (moyoni mwako au mbele ya watu) ndoto yako, bali mkiri Bwana naye atayanyoosha mapito yako, ndugu yangu, rafiki yangu.

Najua katika Biblia watu wa Mungu (kama Yusufu mwana wa Yakobo katika Agano la Kale na mume wa Mariamu Agano Jipya) waliota ndoto, na imeandikwa “na wazee wenu wataota ndoto” (Mat.2:17), lakini ndoto hizo na maono yote ambayo watumishi wa Mungu walikuwa nayo katika Biblia yanahusu mapenzi ya Mungu kwa watu wake na mpango wa Mungu juu ya mambo yajayo – zinatokana moja kwa moja na Mungu Mwenyewe, hazitokani na hamu ya watu ili kuzitumiza ndoto zao! Kama nilivyosema, mafundisho haya hayatofautishi kati ya “shauku zetu binafsi” (‘ndoto’ au ‘maono’ au ‘mtazamo’) kwa ajili ya maisha yetu yajayo na “mapenzi ya Mungu” kwa ajili ya maisha yetu. Na hiki ndicho wahubiri siku hizi wanachofanya – wanatumia kilichotokea,kwa mfano, kwa Yusufu, mwana wa Yakobo, kwenye haja na matamanio binafsi!

Rafiki, kama huelewi au hutambui utofauti kati ya mambo haya mawili, fuate onyo la mtume Paulo katika Warumi 12:1,2 na ujifunze ukweli wa maneno ya Mungu hayo:

“Hili ndilo asemalo BWANA: ‘Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake au mwenye nguvu asijisifu katika nguvu zake au tajiri asijisifu katika utajiri wake, Lakini yeye ajisifuye na ajisifu kwa sababu hili: Kwamba ananifahamu na kunijua mimi, kwamba mimi ndimi BWANA, nitendaye wema, hukumu na haki duniani, kwa kuwa napendezwa na haya,’ asema BWANA.” (Yer.9:23,24).

Mungu alimuahidi Abrahamu mtoto. Abrahamu alisubiri kwa muda mrefu sana ili ahadi hiyo iweze kutimia. Alikuwa bado akisubiri hata pale Mungu alipomtokea kwenye Mwanzo 15 na kusema,

‘Usiogope Abrahamu: mimi ni ngao yako, na ni thawabu yako.’

Abrahamu alikuwa na hofu kwamba bado hakuwa na mtoto, lakini Mungu alimwambia, ‘Mimi ndiye thawabu yako.’ Je hii ni kweli kwangu mimi na wewe, mpendwa msomaji? Unamuhesabu Yesu Kristo kama thawabu yako kubwa, kuliko kitu kingine chochote? Je, Yeye ni wa thamani kwako kuliko hata karama zako au mwito wako? Je, Yeye ni thawabu kubwa kwako kuliko ‘ndoto’ na ‘matamanio’ yako? Kama sivyo, anawezaje kukutumia?

Mungu alimpa Abrahamu mtoto, jina lake Isaka. Mungu alitimiza ahadi yake kwa wakati wake na kwa njia zake. Wakati Isaka bado akiwa mdogo, Mungu akamwambia Abrahamu amtoe sadaka ya kuteketezwa. Abrahamu hakusita. Asubuhi na mapema Abrahamu aliamka kumchukua mtoto kwenye eneo la kutolea sadaka – eneo ambalo hapo baadaye Yesu Kristo alikuja kusulubiwa. Tunahitaji kuelewa ni jinsi gani ile dhabihu ilikuwa kubwa kwa Abrahamu. Si tu Isaka mwanae wa pekee, aliyepewa kimuujiza na Mungu lakini Mungu aliahidi kutengeneza taifa kupitia kwa Abrahamu na kwamba uzao wake utakuwa kama nyota za angani! Mungu alimuahidi Abrahamu kwamba jamaa zote za dunia zitabarikiwa kupitia yeye na uzao wake! Kwa hiyo ahadi za Mungu kwa baraka zijazo ambazo zingekuja kukamilishwa kupitia Isaka, na Abrahamu si kwamba tu alimtoa mwanae wa pekee, ambaye alimpenda, lakini pia kumtoa kama dhabihu ya ahadi zote ambazo Mungu alimuahidia, kama Isaka angekufa, mahadi ya mungu pia ingekuwa imechinjwa!

Inakuwaje kwako? Uko tayari kuweka kando mipango yako binafsi, matamanio ama ndoto kwa hili ama kwa lile ’kwenye madhabahu’ na kusema, si mapenzi yangu bali ya kwake ndiyo yafanyike! Je uko tayari ‘kuachilia’ yale unayotaka kufanya, ama yale unayoyawaza kwamba Mungu amekupangia, na umuache yeye ‘afufue’ kile alichokichagua kwa ajili yako? Abrahamu, alipokwenda kumtoa Isaka, aliwaambia wajakazi wake wasubiri wakati yeye anaenda ‘kuabudu’. Je, unaweza kumuabudu Mungu kwa njia hii – kumfanya yeye ngao yako na thawabu yako kuu, kumpenda yeye kuliko huduma yoyote ama mafanikio ambayo umekuwa ukiyaota? Je, mambo mengine yanaonekana kama si kitu kwako ukilinganisha na kumjua yeye na kumpenda yeye na kutembea katika njia zake? Kama sivyo, atawezaje kukutumia? Kama sivyo, Mungu atawezaje kuwabariki wengine kupitia wewe? Kama ‘tutamwabudu’ Mungu kwa jinsi hii, hatutapoteza! Mungu mwenyewe atatupa kile tunachotaka na kutupa njia tutembee na kubariki wengine kama sisi wenyewe!

Wapendwa, nayaandika hayo kwa sababu tunaishi “wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” (2 Tim.4:3,4). Mungu tusaidie tuwe wafuasi kweli kweli wa Bwana Yesu.

Comments

Popular posts from this blog

Police: Girl, 7, Survives Ky. Plane Crash; Police ID 4 Dead

 A 7-year-old girl survived a plane crash in Kentucky that killed four people Friday night, and the disoriented little girl walked away from the wreckage and reported the crash to a local resident, authorities said. The small Piper PA-34 reported engine trouble and lost contact with air traffic controllers as it was flying over the southwestern part of Kentucky about 5:55 p.m. CST, the FAA said. About a half hour later, a Lyon County resident called 911 and told dispatchers that a 7-year-old girl had walked to his home and said she had been involved in a plane crash, said Sgt. Dean Patterson of the Kentucky State Police. "This girl came out of the wreckage herself and found the closest residence and reported the plane crash," Patterson said. "It's a miracle in a sense that she survived it, but it's tragic that four others didn't." The girl was in emotional distress and taken to a hospital with non-life-threatening injuries, Patterson said. At th...

Kisii Senator Chris Obure and three former Permanent Secretaries charged over corruption related to the multi-billion shilling Anglo Leasing scandal.

Kisii Senator Chris Obure and three former Permanent Secretaries were on Wednesday charged over corruption related to the multi-billion shilling Anglo Leasing scandal. Obure who was charged over crimes committed when he was a Minister of Finance in former President Daniel arap Moi’s government, was in the dock alongside former Transport and Communication Permanent Secretary Sammy Kyungu, former PS Ministry of Finance Joseph Magari and former PS for Internal Security and Provisional Administration Dave Mwangi. They have all denied abuse of office and conspiracy to commit economic crime charges, although Mwiraria and the Kamani’s who are represented by lawyer Ahmednassir Abdullahi were not in court/CFM NEWS Also charged alongside them were former Postmaster General Francis Chahonyo, former Finance Secretary Samuel Bundotich and David Onyonka who was in-charge of debt management in the Ministry of Finance at the time he is accused of committing economic crimes. David Mwiraria who...

Boinett koegwa amatuko emerongo etano nomo komobwata Lengoboini

Ekegambero ekenene kia Nakuru kiamoeire omonene bwa abanyanyimbo omogeni omosike Joseph Boinett amatuko emerongo etano nomo komobeka biara omoriki bw' ekeombe kia abaorokia gia TSC nyumba yogosinywa goakana abaorokia baria batimokire korwa emeremo goakanwa. nigo gekobooria buna abekwe chingayo emetienyi etano nomo emegima ase ogosinywa kobaakana chibillion 16.7 chia aboorokia ang'e 56,000. Rero omokonyi o Inspector General Samuel Arachi nigo aoroka bosio bwa Justice Janet Mulwa koorokia buna ninki gekogera okobwatwa kwa Lengoiboini gwachigetwe omotienyi o kabere chitariki emerongo ebere gotaraikeranigwa na abanyanyimbo.Arachi nigo agoteba abeire abisi ase emeremo ebetereretie chingaki ogochika owko kwarwetwe chitariki 26,na akamanyigwa ekero airanete chitariki isato omotienyi o gatato. Nigo boigo amentire buna onorai oyio nigo abeire isiko y'ense gochakera chitariki 28 omotienyi o kabere koirera okoegwa riuko erio koba egento egekong'u pa.