Skip to main content

TAARIFA YA HABARI 06/04/2015


 -- karibu kwa taarifa zetu jioni/asubuhi hii  wakati wa kupokea habari za yard na AGR fm lakini kwanza tupate mkhutasari wake

--Ni maisha yetu lazima tume ya TSC itujali maslahi  yetu walimu wa --masaba kazikazini wasimama kidete.
--Msipofanya kazi vizuri zitawapatia pesa mwakilishi wa magenche awambia wanakandarasi
--Kanisa zote zaombwa kushirikiana kupambana na madawa za kulevya kisii
hujambo

1 Walimu kutoka wilaya ya Masaba kaskazni wameiomba tume ya kuwaajiri  walimu [TSC] kuwajali  wakati wa kuwahamisha  walimu hao hadi shule zingine.
Akiongea hiyo jana katika  eneo la  Masaba kaskazini kaunti ya Nyamira  mwenyekiti wa walimu kutoka masaba Meshack Obonyo ameiomba tume ya kuwaajiri walimu [TSC] kuzingatia afya na masuala mengine ya walimu kabla ya kuwahamisha  hadi shule  zingine.
Kulingana na Meshack walimu uhamishwa kuenda katika shule zingine ambazo ni mbali kutoka  sehemu wanakoishi   jambo ambalo amesema huwa ngumu kwa walimu hao kwani  kiwango cha pesa wananachokabidhiwa  cha maruburubu ni kidogo mno ambacho hakiwatoshi katika  shughuli zao za kila siku..
Huku  Mwekahazina   Evans Karuru akiomba tume hiyo kuzingatia afya ya walimu  kabla ya kuwahamisha hadi  katika shule zingine.
2 Mwakilishi wa wadi ya Magenche iliyoko eneo bunge la Bomachoge Borabu Kaunti ya Kisii Timothy Ogugu ametishia kurudisha pesa za maendeleo za wadi yake kwa serikali ya kaunti baada ya mwanakandarasi aliyepewa kandarasi ya kujenga zahanati ya Kiabugesi kualibu ujenzi huo na kusema jinsi mwanakandarasi huyo alijenga si halali.
Akizungumza jana katika wadi yake mwakilishi huyo alishangazwa jinsi mwanakandarasi huyo alifanya ujensi wa zahanati hiyo ya Kiabugesi ilyoko wadi yake na kusema atazirudisha pesa hizo kwa serikali ya kaunti au kuanzisha ujenzi huo upya  baada ya kuthibitisha kuwa mwanakandarasi huyo hualibu kazi na kusema hakuna haja ya kukabidhiwa pesa hizo.
Aidha, mwakilishi huyo aliwaonya wanakandarasi wote katika wadi yake ambao hawafanyi kazi kunavyostahili kuchukuliwa hatua ya kisheria kwani pesa zinazotumika ni za mkenya wa kawaida kufanyiwa maendeleo.
.
Mwakilishi huyo alianzisha ujenzi wa zahanati 6 katika wadi yake hiyo jana kwa kutumia pesa hizo za maendeleo huku akiwaonya wanakandarasi kuwa wakialibu ujenzi huo basi hawatapokezwa pesa ila kurudisha kwa serikali pesa hizo au kuanza ujenzi huo upya
Miongoni mwa zahanati alizoanzisha hiyo jana ni Eberege ,Nyabiore,Itembu,Riogachi na Magenche na wakati huo pia alianzisha ujenzi wa madarasa ya ECD katika shule za msingi katika wadi hiyo


3 Baada ya ahadi nyingi za kuboresha huduma za afya katika kaunti ya Kisii, gavana wa Kaunti hiyo James Ongwae mwishowe ametia saini ya ufadhili wa kujengwa kwa kituo cha saratani katika hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii.
Ufadhili huo wa zaidi ya shilingi bilioni 2, fedha hizo zimetolewa na Benki ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika(BADEA), kulishuhudia gavana Ongwae, Henry Rotich waziri wa Fedha  na mkurugenzi mkuu wa benki hiyo ya BADEA Bwa Yousef Ibrahim Al Bassam, Gavana huyo wa Kisii akipokezwa hundi ya hela hizo huko jijini Nairobi.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kutia saini mradi huo jijini Nairobi, Bwa Ongwae alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho utaanza kabla ya mwisho wa mwaka huu ambapo alimshukuru mkurugenzi mkuu wa benki hiyo ya BADEA kwa kufadhili mradi huo wa ujenzi wa kituo ulikuwa mojawapo ya ahadi alizotoa gavana huyo katika harakati za kuboresha na kuimarisha huduma za afya kwa wagonjwa na wale wanaotembelea hospitali ya Kisii .


4 Kasisi wa kanisa ya katholiki katika chuo kikuu cha Kisii Lawrence Nyaanga ameomba kanisa zote kushirikiana na kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya katika jamii.
Akiongea jana, Jumatano katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kisii wakati shirika la Kupambana na madawa ya kulevya nchini NACADA lilipoanzisha mafunzo na fahamisho juu ya hatari ya madawa za kulevya, Nyaanga aliomba kanisa zote kushirikiana kwa pamoja ili kufunza wakaazi kuhusiana na madhara ya madawa hayo
Shirika la kupambana na madawa ya kulevya, NACADA, likishirikiana na chuo kikuu cha Kisii walianzisha kampeini ya siku tatu mfululizo huku siku ya ijumaa itakuwa ni kupita katika barabara za mji wa Kisii ili kuwafahamisha na kuwaelimisha wakazi juu ya hatari ya madawa ya kulevya, huku mwenyekiti wa shirika hilo John Mututho akitarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

Imeandaliwa na Denis zadock mwanahabari wetu ,Peter Onkoba Producer, Brighton Makori Reporter @  yard fm na AGR FM 4th juni  2015

Comments

Popular posts from this blog

Kisii Senator Chris Obure and three former Permanent Secretaries charged over corruption related to the multi-billion shilling Anglo Leasing scandal.

Kisii Senator Chris Obure and three former Permanent Secretaries were on Wednesday charged over corruption related to the multi-billion shilling Anglo Leasing scandal. Obure who was charged over crimes committed when he was a Minister of Finance in former President Daniel arap Moi’s government, was in the dock alongside former Transport and Communication Permanent Secretary Sammy Kyungu, former PS Ministry of Finance Joseph Magari and former PS for Internal Security and Provisional Administration Dave Mwangi. They have all denied abuse of office and conspiracy to commit economic crime charges, although Mwiraria and the Kamani’s who are represented by lawyer Ahmednassir Abdullahi were not in court/CFM NEWS Also charged alongside them were former Postmaster General Francis Chahonyo, former Finance Secretary Samuel Bundotich and David Onyonka who was in-charge of debt management in the Ministry of Finance at the time he is accused of committing economic crimes. David Mwiraria who...

MALLS ACROSS COUNTRY ON HIGH ALERT AFTER AL-QAEDA LINKED TERROR THREAT

A video purported to be by Somalia's al-Qaida-linked rebel group al-Shabab urged Muslims to attack shopping malls in the U.S., Canada, Britain and other Western countries. U.S. authorities said there was "no credible" evidence suggesting a U.S. mall attack was in the works. The threat by the al-Qaida affiliate came in the final minutes of a more than hourlong video released Saturday in which the extremists also warned Kenya of more attacks like the September 2013 assault on the Westgate Mall in Nairobi in which 67 people were killed. The masked narrator concluded by calling on Muslims to attack shopping malls, specifically naming the Mall of America in the Minneapolis suburb of Bloomington, as well as the West Edmonton Mall in Canada and the Westfield mall in Stratford, England. The authenticity of the video could not be immediately verified by The Associated Press. The FBI and Department of Homeland Security provided local law enforcement agencies and private sec...
kisii County News Thursday,June 18 2015 Father jailed for 30 years for killing son A signboard showing directions to Kisii law courts. A father was jailed for 30 years by the High Court in Kisii for killing his son. A man was jailed for 30 years by the High Court in Kisii after he was convicted of murdering his son. Kennedy Obara murdered his two and a half year old son, Hezbon Nyamongo by strangling him on April 11, 2013 at Nyaramba sub location in Gucha South, Kisii County. The court was told that Obara, who had a habit of beating his wife, had beaten her on the fateful night using a walking stick after which she fled to her parents at Suguta. She left behind her two sons who included the deceased and his seven-year-old brother. Kisii Resident Judge Ruth Sitati said that after carefully examining the evidence given by the prosecution and the cross examination, she concluded that it was Obara who killed the deceased. She said that in her considered view there was sufficient...