Prepared by Denis zadock news anchor yard fm 28th may 2015
-- Imetimu saa 4.oopm wakati wa kupokea habari za yard fm lakini kwanza tupate mkhutasari wake
-- Ukidhani umeathirika na ugonjwa wa saratani usikonde kuna kupimwa na kushugulikiwa kikamilifu asema waziri wa afya kisii saraha omache
-- Tuliamurishwa kufunga shule kutokana na hali mbaya ya vyoo asema mwalimu mkuu wa shule ya gesere D.O.k
-- Mwakilishi wa wadi Fred menge amrudishia asante rais Kenyatta kwa kupunguza gharama ya stima
-- Hatutakubali wakulima kuendelea kutezeka afisa wa benki ya dunia Charles mochama aambia serikali ya Nyamira
-- Hujambo na karibu naitwa …………………..
1 Maafisa wa afya kutoka kaunti ya Kisii wamefunga Shule ya msingi ya Gesere D.O.K iliyoko wadi ya Ibeno kaunti ya Kisii hadi wakati usiojulikana kufuatia na vyoo vya shule hiyo kuwa katika hali mbaya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mwalimu mkuu wa shule hiyo Velster Onchari alisema maafisa wa afya kutoka kaunti ya Kisii walienda hadi shuleni humo na kuamrisha shule kufungwa kwa kile walichokitaja vyoo vya shule hiyo kuwa katika hali mbaya na huenda wanafunzi waathirike na ugonjwa wa kibindubindu.
Shule nyingi katika eneo la Kisii zimekuwa zikifungwa kutokana na vyoo vibaya ambavyo hulazimu maafisa wa afya kufunga shule hizo
2 Waziri wa afya katika kaunti ya Kisii Sarah Omache amesema madaktari kutoka hospitali ya PLK iliyoko nchini India watakuja tarehe mosi mwezi ujao katika hospitali ya rufaa ya Kisii kupima watu ugonjwa wa sukari na saratani na kuomba watu kujitokeza kwa wingi kupimwa siku hiyo hiyo ya Madaraka.
Akiongea na wanahabari hiyo jana katika hospitali ya rufaa ya Kisii Omache alisema baada ya gavana James Ongwae na baadhi ya maafisa kutembelea nchi ya India kuona jinsi huduma za matibabu kwa sekta ya afya hutolewa ndiposa aliongea na madaktari wa hospitali hiyo ya PLK na kuwaalika Kisii kuwapima watu magonjwa hayo na wakakubali kufanya hivyo.
Wakati uo huo waziri huyo alisema dalili za magonjwa hayo mwilini ni kutoka damu kutoka kwa mwili,kusikia uchungu mtu anapomeza chakula pamoja na choto nyingi.
Sasa madaktari hao watafika Kisii baada ya serikali ya kaunti ya Kisii kuweka mkataba wa maelewano na hospitali ya PLK na watafika kisii kufanya huduma hiyo tarehe 1/6 mwaka huu hayo ni kwa mujibu wa waziri wa afya kaunti ya kisii Saraha Omache
3 Mwakilishi mteule wa wadi katika kaunti ya Nyamira Fred Menge amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kupunguza gharama ya kuunganishwa kwa nguvu za umeme kwa wananchi kutoka shillingi alfu 35 hadi shillingi alfu 15
Akizungumza na waandishi wa habari hiyo jana katika mji wa Nyamira mwakilishi huyo alisema kuwa Rais Kenyatta aliwajali wananchi kwa kupunguza gharama ya kuunganisha stima
Kwa upande mwingine wakaazi wa kaunti ya Nyamira nao hawakuachwa nyuma kwa kuunga mkono mwakilishi huyo kumpigia asante rais Kenyatta kwa kile alichofanya kwa kupunguza gharama hiyo ya stima.
Sasa kuunganishiwa stima ni shillingi alfu 15 ikilinganishwa na shillingi alfu 35 za hapo mbeleni
4 Vijana wanaochimba mawe na kutengeneza kokoto katika timbo la mawe lililoko Daraja Mbili viungani mwa mji wa Kisii, wamelalamikia maji ya mvua ambayo yanawatatiza msimu huu wa mvua .
Vijana hao ambao hupata riziki yao kupitia shughuli hiyo ya kuponda mawe kuwa kokoto, walitaja mvua kuwa kikwazo ambapo walisema kuwa maji yamekuwa kero kwani yanajaa kwenye timbo hilo na kuwatatiza.
Wachongaji mawe hao kupitia kwa mwenyekiti wao Andrew Ondega, waliomba serikali ya kaunti kisii kuwatafutia suluhu la maji hayo ambayo huwatatiza na kuwakwaza kutekeleza shughuli zao ipasavyo.
Aidha mwenyekiti huyo aliitaka serikali ya Kaunti kuwajali na kuwanunulia vifaa muhimu vya kuwawezesha kufanya kazi yao kwa njia salama ambapo alisema kuwa wamekuwa wakiumizwa na mawe hayo kwenye viungo hasa macho.
5Afisa wa benki ya dunia Charles Mochama ameomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuwa na kikao na wakurugenzi wa viwanda vya majani chai vya kaunti ya Nyamira kutafuta suluhu ya wakulima kupata hasara kwa kutochukuliwa kwa majani chai yao kutoka kwa vituo vya kupima
Akizungumza na wanahabari katika mji wa Nyamira afisa huyo wa benki ya dunia alisema Wakulima wamepata hasara kubwa kwa kutochukuliwa kwa majani chai yao kutoka vituoni mpaka majani hayo hualibika .
Afisa huyo ameomba serikali ya kaunti ya Nyamira na washkadau wote wa sekta ya majani chai kujiunga pamoja kuandaa kikao kutafuta suluhu mwafaka kutokana changamoto ambazo wakulima hupitia baada ya wakulima kuendelea kupata hasara kubwa .
Comments
Post a Comment